Monday, November 2, 2015

COSTA CHUPUCHUPU KUADHIBIWA NA FA.

CHAMA cha Soka cha Uingereza-FA hakitamchukulia hatua za kinidhamu mshambuliaji Diego Costa baada ya kuonekana akimkwatua Martin Skrtel katika mchezo baina ya timu hizo uliochezwa Jumamosi iliyopita. Mwamuzi wa mchezo huo Mark Clattenburg ililiona tukio hilo lakini badala yake alitoa onyo pekee kwa nyota huyo hivyo kumaanisha kuwa hakuna adhabu yeyote itakayotolewa na mamlaka. Wachezaji hao wawili walianguka chini baada ya fauli hiyo iliyochezwa na nyota huyo wa kimataifa wa Hispania. Akihojiwa mwamuzi wa zamani aliyechezesha fainali za Kombe la Dunia Howard Webb amesema kwa upande wake tukio hilo lilikuwa kadi ya wazi kabisa. Webb amesema Costa alimfanyia faulo Skrtel na baadae kumpiga teke kidogo hivyo kwa tukio la pili anadhani ni ukosefu wa nidhamu hivyo ana bahati kupewa onyo pekee.

No comments:

Post a Comment