MSHAURI wa rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter amesema kulifanyika makubaliano ya kuipa Urusi uenyeji wa michuano ya Kombe la dunia mwaka 2018 kabla ya kura hazijafanyika zilizowahusisha wakubwa wa shirikisho hilo. Mshauri huyo Klaus Stohlker amesema kulikuwa na mazungumzo ya nyuma ya pazia yaliyowahusisha wajumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA. Blatter ambaye amesimamishwa kwa siku 90 alibainisha kuwa kulikuwa ba maelewano ya kutoa uenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2022 kwa Urusi na Marekani. Michuano ya mwaka 2022 baadae walipewa Qatar baada ya kura kubadilika. Suala ya uenyeji wa michuano ya mwaka 2018 na 2022 ni jambo ambalo linafanyiwa uchunguzi na mamlaka nchini Uswisi wakishirikiana na Marekani.
No comments:
Post a Comment