Monday, November 30, 2015

KLOPP AFURAHIA KUREJEA KWA STURRIDGE NA HENDERSON.

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amefurahishwa kuwa nao tena Daniel Sturridge na Jordan Henderson haswa katika kipindi hiki ambacho ratiba ya mechi za ligi huwa ngumu. Wawili hao walirejea jana katika benchi la wachezaji wa akiba katika mchezo mgumu ambao Liverpool walishinda bao 1-0 dhidi ya Swansea City jana. Henderson aliyekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya mguu na Sturridge goti, yaliwafanya kukaa nje kwa kipindi kirefu lakini sasa wamerejea katika wakati muhimu ambao Liverpool itakabiliwa na mechi nne ndani ya siku 12. Klopp amesema kurejea kwa wawili hao ni taarifa njema kwao kwani ni wachezaji muhimu na wamerejea wakati muafaka.

No comments:

Post a Comment