Monday, November 30, 2015

WENGER AJIPA MATUMAINI NA UBINGWA WA LIGI KUU.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger ana uhakika kikosi chake bado kipo katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na kukiri kupitia wakati mgumu. Arsenal walilazimishwa sare na Tottenham Hotspurs kabla ya kufungwa na ambao 2-1 na West Bromwich Albion wiki iliyopita na jana tena kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Norwich City. Wenger amekubali kuwa walipaswa kupata matokeo mazuri zaidi ya hayo lakini kutokana na Arsenal kuwa nyuma kwa alama mbili dhidi ya vinara Manchester City na Leicester City, kocha huyo Mfanrasa anaamini haina haja ya kuhamaki. Wenger amesema kwasasa wanapitia kipindi kigumu kwani wameshindwa kupata matokeo mazuri katika mechi zao tatu zilizopita za ligi lakini hana hofu kwakuwa hawajaachwa mbali sana.

No comments:

Post a Comment