Monday, November 30, 2015

VILABU URUSI VYAFUNGIWA KUSAJILI WACHEZAJI KUTOKA UTURUKI.

KLABU za Urusi zinatarajiwa kufungiwa kusajili wachezaji kutoka Uturuki katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo Januari mwakani. Mahusiano kati ya nchi hizo yamekuwa yakizorota toka ndege ya kivita ya Urusi itunguliwe na majeshi ya Uturuki katika mpaka wa Syria na kuua pailoti mmoja. Waziri wa Michezo wa Urusi Vitaly Mutko amesema tayari ujumbe umeshapelekwa kwa vilabu kuwa haitawezekana kwao kusajili wachezaji kutoka Uturuki katika kipindi cha usajili kinachokuja. Mutko aliendelea kudai kuwa vikwazo hivyo havitaweza kuathiri wachezaji wa Uturuki ambao tayari wanacheza soka nchini humo akiwemo kiungo wa Rubin Kazan Gokdeniz Karadeniz ambaye alijiunga nao mwaka 2008. Mutko amesema yeyote ambaye ana ana mkataba unaoendelea ataendelea kufanya kazi kama kawaida.

No comments:

Post a Comment