Monday, November 30, 2015

ETOILE DU SAHEL MABINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO.

KLABU ya Etoile Du Sahel ya Tunisia imefanikiwa kuichapa Arlando Pirates ya Afrika Kusini kwa bao 1-0 katika mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho uliochezwa jana katika Uwanja wa Olimpiki huko Sousse. Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na nahodha Ammar Jemal na kuifanya Etoile kuibuka ushindi wa jumla wa mabao 2-1 kufuatia timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wao wa kwanza uliochezwa Soweto Jumamosi iliyopita. Mchezo huo ulichezwa chini ya ulinzi mkali kufuatia shambulio la bomu lililotokea jijini Tunis huku mashabiki wakipunguzwa na muda mchezo kuwekwa mapema zaidi kuliko ulivyopangwa awali. Ushindi huo umeifanya Etoile kukunja kitita cha dola 660,000 pamoja na nafasi ya kucheza mchezo wa Super Cup dhidi ya mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC.

No comments:

Post a Comment