Monday, November 30, 2015

KOBE BRYANT KUSTAAFU KIKAPU MWAKANI.

MCHEZAJI nyota wa Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani-NBA, Kobe Bryant ambaye anahesabiwa kama mmoja ya wachezaji bora kabisa katika historia, anatarajiwa kustaafu mchezo huo mwishoni mwa msimu. Bryant amefunga vikapu 32,683 katika kipindi cha miaka 20 alichoichezea timu ya Los Angeles Lakers na kumfanya kushika nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji wa wakati wote wa NBA. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 37 ambaye ana medali za dhahabu za mashindano ya Olimpiki, amekuwa akisumbuliwa na majeruhi katika misimu ya karibuni na kumfanya kuwa chini ya kiwango msimu huu akiwa na Lakers. Bryant alitajwa kama Mchezaji Mwenye Thamani Zaidi wa NBA mwaka 2008 na amewahi kuchaguliwa katika kikosi cha NBA All-Star kwa nyakati 17 tofauti. Mchezo wa mwisho wa Bryant unatarajiwa kuwa dhidi ya Utah Jazz utakaochezwa Aprili 13 mwakani.

No comments:

Post a Comment