Wednesday, November 18, 2015

KLUIVERT AITAMANI BARCELONA.

NGULI zamani wa soka wa Uholanzi, Patrick Kluivert yuko tayari kuanza kibarua cha ukocha katika soka na ana matumaini ya kurejea Barcelona siku moja. Kluivert yuko katika hatua za mwanzo za ukocha akiwa amefanya kazi kama kocha msaidizi wa Uholanzi chini ya Louis van Gaal katika Kombe la Dunia mwaka 2014. Nguli huyo kwasasa anafanya kazi ya ushauri katika timu ya taifa ya Curacao kutoka visiwa vya Caribbean huku akitafuta kibarua katika vilabu. Akihojiwa Kluivert amesema malengo hivi sasa ni kutafuta klabu ya kufundisha na bado ana matumaini ya kuinoa Barcelona ingawa anafahamu haitakuwa hivi karibuni. Akiwa mchezaji Kluivert amewahi kuitumikia Barcelona kwa miaka sita.

No comments:

Post a Comment