Friday, November 20, 2015

KOSCIENY HATIHATI KUIVAA WEST BROM KESHO.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa beki wa kati Laurent Koscielny ameathirika kwa kiasi kikubwa na tukio la mashambulio lililotokea jijini Paris na anaweza kumpumzisha katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya West Bromwich Albion kesho. Koscielny alikuwepo katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kilichokuwa kikicheza na Ujerumani huko Stade de France wakati tukio la mashambulio hayo lilipotokea na wakati wakicheza na Uingereza Jumanne, Wenger alibaini kuwa akili ya mchezaji huyo ilikuwa mahali pengine. Akihojiwa Wenger amesema Koscielny alicheza vyema katika mchezo dhidi ya Ujerumani lakini kwa jinsi alivyomuona katika mchezo wa Jumanne usiku hakuwa mwenyewe. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa anadhani ameathirika kwa kiasi kikubwa hivyo hatafanya haraka kumtumia mpaka atakaporidhika kwamba yuko tayari.

No comments:

Post a Comment