MANCHESTER UNITED MBIONI KUVUNJA REKODI YA MAPATO.
KLABU ya soka ya Manchester United imetangaza mapato yao ya robo ya Kwanza ya Mwaka wa Kifedha. Klabu hiyo pia iko mbioni kuvunja rekodi ya kuvuka mapato ya paundi milioni 500 na kuweka rekodi ambayo hajafikiwa na klabu yeyote. Mapato ya United kwa miezi mitatu, iliyoiishia Septemba, ni paundi milioni 123.6 ikiwa ni ongezeko la asilimia 39 kwa kipindi kama hiki kwa mwaka 2014. Pia mapato yameongezeka baada ya kusaini mkataba mpya na kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas ambayo yatawaingizia paundi milioni 750 kwa miaka 10 ukiwa ni mkataba mkubwa kabisa Duniani kwa klabu na Watengeneza Vifaa vya Michezo. Vilevile, kushiriki kwa timu hiyo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kumechangia ongezeko la pato lao kwenye matangazo ya mechi kwa asilimia 64.3. Asilimia 64.2 hutokana na viingilio vya mashabiki pamoja na kuuzwa kwa bidhaa nyingine zikiwemo jezi.
No comments:
Post a Comment