Friday, November 13, 2015

RONALDO ANA MARAFIKI WACHACHE MNO.

MTAYARISHAJI wa filamu inayoelezea maisha ya mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema nyota huyo anaishi maisha ya upweke mno. James Gay-Rees ambaye alipata umaarufu kwa kuandaa filamu kuhusu ya maisha ya dereva mahiri wa mashindano ya langalanga Senna, raia wa Brazil, amesema kuwa Cristiano hana marafiki wengi. Gay-Rees amesema mara nyingine nyota huyo hupenda kutumia muda wake mwingi akiwa na familia yake. Mtayarishaji huyo aliendelea kudai kuwa anadhani kikubwa kinachochangia Ronaldo kuwa na marafiki wachache ni kule kujituma kwake kwani kunamhitaji kuwa na nidhamu ya hali ya juu. Gay-Rees amesema kwa hadhi kama ya Ronaldo anapaswa kuwa mnyeyekevu wa kupindukia ili aweze kubaki katika kiwango cha juu kama anayofanya.

No comments:

Post a Comment