NAHODHA wa timu ya taifa ya Uholanzi, Arjen Robben amesema mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Wales ni nafasi ya kuanza kujijenga upya baada ya kushindwa kufuzu michuano ya Euro 2016. Uholanzi walishindwa kufuzu michuano hiyo kwa kumaliza katika nafasi ya nne katika kundi lao pamoja na kupangwa kama timu ya juu. Robben mwenye umri wa miaka 31, toka wakati huo amechukua beji ya unahodha kutoka kwa Robin van Persie na anataka kuanza kwa kuifunga Wales ambao wamefuzu michuano hiyo. Akihojiwa Robben amesema jambo pekee wanaloweza kufanya ni kujaribu na kuwanza kujijenga upya tayari kwa maandalizi ya mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018. Robben aliendelea kudai kuwa pamoja na kwamba ni kipindi kirefu lakini inabidi wakabiliane na ukweli na kupata matokeo mazuri katika mechi zao zinazokuja.
No comments:
Post a Comment