Friday, November 13, 2015

IBRAHIMOVIC ATAMBA KUIWEKA UFARANSA KATIKA RAMANI YA SOKA.

MSHAMBULIAJI nyota wa Paris Saint-Germain-PSG, Zlatan Ibrahimovic amedai kuwa umahiri wake wa kufunga mabao umeiweka Ufaransa katika ramani. Ufaransa wamewahi kushinda taji la Kombe la Dunia mwaka 1998 katika ardhi yao wenyewe, lakini Ibrahimovic anaamini mabao 115 aliyoifungia PSG yamesaidia kuiweka nchi hiyo katika ramani nzuri kisoka. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 54, ambaye amefunga mabao 59 katika mechi 109 alizoichezea nchi yake ya Sweden, amesema anafurahia kuhusu suala hilo. Ibrahimovic aliendelea kutamba kuwa amekuwa akicheza huko kwa miaka minne, ameiweka Sweden katika ramani ya dunia na sasa amefanya hivyo kwa Ufaransa pia. Sweden inajiandaa kwa ajili ya mchezo wa mtoano dhidi ya Denmark kesho ambapo mshindi atakuwa amepata nafasi ya kushiriki michuano ya Euro 2016.

No comments:

Post a Comment