RONALDO AJIWEKA SOKONI AKIDAI HANA MPENZI KWASASA.
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo amebainisha kuwa hana mpenzi kwasasa na wako wachache wanawake wachache wanaopigania penzi lake. Nyota huyo aliachana na mpenzi wake wa siku nyingi Irina Shayk mapema mwaka huu na amekwua akihusishwa kuwa na mahusiana na warembo kadhaa toka wakati huo. Hata hivyo, Ronaldo amekiri kuwa bado hajaamua ni mwanadada yupi atakuwa mpenzi wake na kuongeza imekuwa vigumu kumpata mwanamke ambaye hahitaji umaarufu wake. Ronaldo amesema asilimia 50 ya wanawake wanaomfuata wanamtaka kwa ajili ya umaarufu wake lakini suala hilo halimpi shida kwani watu maarufu wote wanapata matatizo kama hayo. Ronaldo na Shayk ambaye ni mwanamitindo wa Urusi walianza uhusiano wao mwaka 2010 lakini walitengana Januari baada ya mwanadada huyo kumtuhumu mwanasoka huyo kutokuwa mwaminifu.
No comments:
Post a Comment