Tuesday, November 10, 2015

MO FARAH ATAKA KUMPA MWANE WA KIUME JINA LA ARSENAL.

MWANARIADHA nyota bingwa wa mashindano Olimpiki wa Uingereza, Mo Farah amebainisha kuwa anataka jina la kati la mtoto wake wa kiume kuwa Arsenal kunatokana na mapenzi makubwa aliyponayo kwa klabu hiyo yenye maskani yake Kaskazini mwa London. Mipango ya Farah inaweza kukwamishwa na mke wake Tania ambaye hataki mwanae huyo aitwaye Hussein kuitwa jina hilo. Akihojiwa Farah amesema ana mapenzi makubwa na Arsenal mpaka anatamani kumpatia mwanae jina hilo lakini mke wake hataki. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa wakati anakua hakutegemea kama anaweza kuwa bingwa mara mbili wa olimpiki, nyuma nzuri na watoto wazuri.

No comments:

Post a Comment