TANZANIA imekwea kwa nafasi moja katika viwango vipya vitolewavyo kila mwezi na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA huku Uganda wakiendelea kuongoza kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati. Kwa orodha hiyo iliyotolewa leo Tanzania ndio wanaoburuza mkia kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki wakishika nafasi ya 53 kwa upande wa Afrika huku majirani zutu Uganda wakiwa nafasi ya 14 na duniani wa 68, Rwanda nafasi ya 23 duniani wa 96, Kenya nafasi ya 48 duniani 125 na Burundi nafasi ya 40 duniani 107. Katika tano bora kwa upande wa Afrika, Ivory Coast ndio wanaoongoza kwasasa wakishikilia nafasi ya 22 wakifuatiwa na Algeria walioko nafasi ya 26, Ghana ni watatu wakiwa nafasi ya 30. CapeVerde wamekwea tena na kuingia tano bora za Afrika kwa kushikilia nafasi ya 32 duniani wakifuatiwa na Senegal walioko nafasi ya 39. Kwa ujumla duniani orodha hiyo sasa inaongozwa na Ubelgiji walioikwaa nafasi hiyo kutoka kwa Argentina ambao wameporomoka mpaka nafasi ya tatu, mabingwa wa dunia Ujerumani wao wako nafasi ya pili, Ureno nafasi ya nne na tano bora inakamilishwa na mabingwa Copa Amerika Chile.
No comments:
Post a Comment