Thursday, November 19, 2015

NASRI NJE MPAKA FEBRUARI.

KIUNGO wa Manchester City, Samir Nasri ametangaza kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa hategemei kucheza mechi yeyote ya kimashindano katika miezi mitatu ijayo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 alipata majeruhi ya msuli katika mchezo wa Ligi Kuu walioshinda mabao 5-1 dhidi ya Bournemouth mwezi uliopita. Meneja wa City, Manuel Pellegrini alikuwa na matumaini kuwa Mfaransa huyo angeweza kurejea uwanjani katika mchezo wao dhidi ya Liverpool mwishoni mwa wiki hii. Lakini sasa matumaini hayo yanaonekana kufifia baada ya kiungo huyo kuweka wazi hataweza kurejea uwanjani mpaka Februari mwakani.

No comments:

Post a Comment