Thursday, November 19, 2015

BALOTELLI KUKAA NJE MWEZI ZAIDI.

MSHAMBULIAJI wa AC Milan, Mario Balotelli anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki nne zaidi baada ya kufanyiwa upasuaji wa nyonga.  Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye yuko kwa mkopo akitokea Liverpool, hajaichezea Milan mechi yeyote toka Septemba 27 kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua. Mara baada ya upasuaji, Balotelli aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akishukuru kwa upasuaji kwenda salama na kuwaahidi mashabiki wake kuwa atarejea hivi karibuni. Balotelli ameichezea Milan mechi nne pekee toka arejee kwa mara ya pili na kufunga bao moja.

No comments:

Post a Comment