Thursday, November 19, 2015

PATO MGUU NDANI MGUU NJE BRAZIL.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa AC Milan, Pato anamaliza mkataba wake wa mkopo katika klabu ya Sao Paulo mwezi ujao na rais wa klabu mama ya Corinthians Roberto de Andrade hivi karibu amesema anaomba amuuze nyota huyo. Pato ambaye alikuwa akihusishwa na tetesi za kwenda Borussia Dortmund na Liverpool, amesema atakuwa akishangilia timu ya Palmeiras katika mchezo wa fainali wa Kombe la Brazil dhidi ya Santos, pamoja na kwamba matokeo yanaweza kuathiri nafasi ya Sao Paulo katika michuano ya Copa Libertadores mwakani. Akihojiwa Pato amesema Santos ni klabu kubwa lakini yeye anatarajia kuinga mkono Palmeiras kwasababu rais wake Paulo Nobre ni mtu mzuri na amefanya kazi kubwa kluijenga timu hiyo. Pato aliendelea kutetea uamuzi wake huo kuwa hauhusiani na yeye kujipigia chapuo ya kujiunga nao kwani hajazungumza nao chochote.

No comments:

Post a Comment