Thursday, November 19, 2015

CLASICO KUSIMAMA DAKIKA MOJA KUOMBELEZA WALIOPOTEZA MAISHA PARIS.

WACHEZAJI na mashabiki watakaohudhuria mchezo wa mwishoni mwa wiki wa Clasico kati ya Real Madrid na Barcelona katika Uwanja wa Santiago Bernabeu watasimama kwa dakika moja kutoa heshima kwa wahanga wa tukio la mashambulio ya kigaidi jijini Paris. Mchezo huo unaozikutanisha klabu hasimu katika La Liga unakadiriwa kutizamwa na watu zaidi ya milioni 500 ikiwa ndio mechi ya vilabu inayotizamwa zaidi duniani. Katika taarifa iliyotolewa imedai kuwa kutakuwa na dakika moja za kukaa kimya kuwakumbuka wahanga hao kabla ya kuanza kwa mchez huo wa Jumamosi ambao utahudhuriwa na watu 81,000. Wakati wa kukaa kimya dakika moja klabu zote zitakuwa na mabango yenye maandishi yanayosomeka kuwa Sisi Sote Ni Wafaransa ambayo pia yataonekana katika picha za video kwa wale wasiokuwepo uwanjani.

No comments:

Post a Comment