Thursday, November 5, 2015

RAIS WA DORTMUND ATUPA TAULO KWA KUINYOOSHEA MIKONO BAYERN.

OFISA mkuu wa Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke amedai klabu yao haiwezi kushindania taji la Bundesliga na Bayern Munich. Dortmund imekuwa katika kiwango kizuri toka ujio wa meneja mpya Thomas Tuchel wakishika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi huku wakipoteza mchezo mmoja pekee katika mashindano yote msimu huu, ingawa mchezo huo ukiwa ule waliotandikwa mabao 5-1 na Bayern. Bayern kwasasa ndio wanaongoza ligi wakitofautiana na Dortmund kwa alama tano na Watzke anaamini mbio za ubingwa zimeshakwisha. Akihojiwa Watzke amesema haina maana yeyote kuzungumzia kuhusu kuifukuzia Bayern kwani mpaka sasa wameshapoteza alama pekee na kama wakiendelea hivyo wanaweza kuendelea kutanua pengo la alama hadi kufikia nane kwa msimu wote. Watzke aliendelea kudai kuwa wanachoangalia wao kwasasa ni jinsi wanavyofanya kwani wameimarika sana toka ujio wa kocha mpya. Dortmund watakuwa wenyeji wa Qabala katika mchezo wa Europa League baadae leo kabla ya kurejea Jumapili hii katika Bundesliga kwa kukwaana na mahasimu wao wa Ruhr Schalke.

No comments:

Post a Comment