MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Real Madrid, Karim Benzema amewekwa rasmi chini ya uchunguzi leo akihusishwa na tuhuma za kulaghai ili kupata pesa kutoka kwa Mfaransa mwenzake Mathieu Valbuena wakitumia mkanda wa video wa ngono. Taarifa ya waendesha mashitaka wa Versailles imedai kuwa tuhuma hizo za kihalifu ambazo zinachunguzwa inaweza kubeba adhabu ya miaka siyopungua mitano jela. Wakili wa Benzema, Sylvain Cormier aliwaambia wanahabari baada ya kusikilizwa kwa shitaka hilo kuwa mteja wake alikuwa hana hatia na hakuhusika kwa vyovyote vile na tukio hilo la kihalifu. Kesi hiyo imeanza kuleta wasiwasi juu ya ushiriki wa mchezaji huyo katika michuano ya Euro 2016 ambayo itafanyika nchini Ufaransa.
No comments:
Post a Comment