Wednesday, November 18, 2015

RUFANI YA BLATTER NA PLATINI YAPIGWA CHINI.

RUFANI ya rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter na makamu wake Michel Platini ya kupinga kufungiwa siku 90 zimetupiliwa mbali na kamati ya rufani ya shirikisho hilo. Wawili hao walisimamishwa Octoba mwaka huu kupisha kamati ya maadili ya FIFA kuendelea na uchunguzi wake dhidi ya tuhuma za rushwa zinazowakabili. Blatter anatuhumiwa kusaini mkataba usiokuwa na manufaa kwa FIFA na kufanya malipo yasiyoeleweka kwa rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA Michel Platini. Viongozi hao wote wamekanusha kufanya jambo lolote baya katika tuhuma hizo zinazowakabili.

No comments:

Post a Comment