Thursday, November 19, 2015

WACHEZAJI MASHOGA RUKSA LIGI KUU.

MWENYEKITI wa Ligi Kuu ya Uingereza, Richard Scudamore amesema wanasoka mashoga watapewa heshima kama wataamua kuweka wazi mambo yao. Akihojiwa na BBC, Scudamore alidai kuwa mazingira yatakuwa rafiki wakati wote kwao pindi wataapojitokeza hadharani. Kumekuwa hakuna mchezaji soka soka yeyote aliyejitangaza kuwa shoga kwa upande wa wanaume nchini Uingereza toka mshambuliaji wa zamani wa Norwich City Justin Fashanu alipojitangaza mwaka 1990. Gazeti la Daily Mirror limeripoti kuwa wako wachezaji wawili wa soka wa ligi za juu wanajipanga kujitangaza kuwa mashoga huku wakiungwa mkono na klabu zao. Nahodha wa timu ya taifa ya wanawake ya Uingereza Casey Stoney ndio mwanasoka wa kwanza kujitangaza kushiriki mapenzi ya jinsia moja Februari mwaka jana toka Fashanu alipofanya hivyo. Kiungo wa zamani wa Aston Villa Thomas Hitzlsperger alibainisha kushiriki mapenzi ya jinsi moja mwaka jana baada ya kustaafu soka na Scudamore ana uhakika kuwa wapo wachezaji mashoga katika klabu za Ligi Kuu.

No comments:

Post a Comment