SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA, limebainisha kuwa mechi zake za Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League zitaendelea kama zilivypangwa wiki ijayo. Ratiba ya michezo mingi ilisimamishwa au kusogezwa mbele maeneo mengi ya Ulaya kufuatia mashambulio ya kigaidi yaliyofanyika jijini Paris Ijumaa iliyopita. Mchezo wa kirafiki kati ya Ujerumani na Uholanzi uliokuwa uchezwe jijini Hannover Jumanne nao ulifutwa dakika za mwisho baada ya taarifa za kuwepo kwa tishio la bomu. Msemaji wa UEFA amesema shirikisho hilo linafanya kazi kwa karibu na klabu zitakazokuwa nyumbani pamoja na mamlaka husika ili kuhakikisha taratibu muhimu zinafuatwa kuhakikisha usalama wa watu wote. Msemaji huyo aliendelea kudai kuwa bado hawajalijadili suala la mashabiki watakaosafiri kwani hilo linahusu mamlaka husika kutoa maamuzi.
No comments:
Post a Comment