WACHEZAJI wote 23 wa kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kimesafiri kuelekea nchini Uingereza leo baada ya kukataa wazo la kutocheza mchezo wao wa kirafiki kufuatia mashambulio yaliyofanyika jijini Paris. Mpwa wa kiungo Lassana Diarra, Asta Diakite ni mmoja ya watu 129 waliouawa Ijumaa iliyopita wakati dada yake mshambuliaji Antoine Griezmann yeye alifanikiwa kutoka salama katika Ukumbi wa Bataclan ambapo watu 89 waliuawa. Wachezaji wote hao walikuwepo katika kikosi cha Ufaransa kilichokuwa kikicheza na Ujerumani katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Stade de France mahali ambapo pia palilengwa na magaidi. Pamoja maswahiba hao wachezaji hao na wengine wote watakuwepo katika mchezo huo wa kirafiki utakaofanyika katika Uwanja wa Wembley kesho.
No comments:
Post a Comment