MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uholanzi, Dick Kuyt amebainisha alikuwepo Disneyland Paris muda huohuo ambao magaidi walishambulia viunga kadhaa vya mji mkuu huo wa Ufaransa. Zaidi ya watu 120 waliuawa na wengine 99 kuachwa katika hali mbaya Ijumaa iliyopita, huku Uwanja wa Stade de France ambao timu ya taifa ya nchi hiyo ilikuw ikicheza na Ujerumani mchezo wa kirafiki ikiwa moja ya maeneo yaliyoshambuliwa. Wakati wa matukio hayo yakiendelea Kuyt ambaye kwasasa anakipiga katika klabu ya Feyenoord alikuwa na familia yake wakiendelea kufurahia mapumziko yao huko Disney. Akihojiwa Kuyt amesema watu wake wengi wa karibu walikuwa wakifahamu kuwa yuko Paris hivyo baada ya kusikia tukio hilo walitafuta kupitia simu yangu lakini haikupatikana kwasababu alikuwa ameizima. Lakini baadae kwa kutumia simu ya mke wake aliwafahamu watu wake wote wa karibu kuwa yuko salama wasihofu. Kuyt aliendelea kudai kuwa eneo alilokuwepo ilikuwa ni kilometa 20 kutoka mahali mashambulio yalipofanyika hivyo hakupata wasaa wa kujua ukubwa wa tatizo mpaka aliporejea hotelini na kuona taarifa.
No comments:
Post a Comment