SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF jana limetoa ratiba kamili ya makundi ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani maarufu kama CHAN itakayofanyika nchini Rwanda mwakani. Michuano hiyo mahsusi kwa wachezaji wanaocheza soka katika ligi za ndani itashirikisha nchi 16 ambazo zimegawnywa katika makundi manne. Wenyeji Rwanda wao wapo katika kundi A sambamba na Gabon, Morocco na Ivory Coast na mechi zao zitachezwa katika Uwanja wa Amahoro jijini Kigali. Mabingwa wa kwanza wa CHAN mwaka 2009 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC wao wapo kundi kundi B sambamba na Angola, Cameroon na Ethiopia ambapo mechi zao zitachezwa huko Butare. Kwa upande wa kundi C litakuwa na mabingwa wa mwaka 2011 Tunisia pamoja na Nigeria, Niger na Guinea wanaoshiriki kwa mara kwanza na watakuwa wakitumia Uwanja wa Nyamirambo uliopo Kigali pia. Kundi D ambalo litakuwa na timu za Zimbabwe, Mali, Uganda na Zambia wao mechi zao zitachezwa huko Gisenyi. Michuano hiyo inatarajiwa kunza kutimua vumbi kuanzia Januari 16 mpaka Februari 7.
No comments:
Post a Comment