NAKHID AKATA RUFANI CAS KUFUATIA JINA LAKE KUKATWA FIFA.
MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Trinidad na Tobago, David Nakhid amekata rufani katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS kufuatia Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kukata jina katika kinyang’anyiro cha urais. Nakhid aliwasilisha maombi yake huku kukiwa sahihi tano za mashirikisho yanayomuunga mkono lakini FIFA walishindwa kupitisha jina lake kutokana na shirikisho moja kati ya aliyowasilisha kumuunga mkono mgombea mwingine. Nakhid sasa amekata rufani CAS akiwa na matumaini kuwa ataweza kusimamishwa katika kinyang’anyiro hicho cha uchaguzi utakaofanyika Februari mwakani. Mpaka sasa wagombea watano majina yao ndio yamepitishwa kugombea nafasi hiyo ambayo ni Prince Ali al-Hussein, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa, Jerome Champagne, Gianni Infantino na Tokyo Sexwale.
No comments:
Post a Comment