Wednesday, November 25, 2015

WARRIORS WAWEKA REKODI YA KUTOFUNGWA NBA.

TIMU ya Golden State Warriors imeweka rekodi ya kutofungwa toka kuanza kwa msimu mpya wa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani-NBA kwa ushindi mnono dhidi ya Los Angeles Lakers. Warriors walishinda mchezo huo uliofanyika jana kwa vikapu 111-77 na kuongeza rekodi yao nzuri ya ushindi katika mechi 16 walizocheza za NBA mpaka sasa. Ushindi huo unamaanisha Warriors wamevunja rekodi ya pamoja iliyowekwa na Houston Rockets msimu wa 1993-1994 pamoja na Washington Capitals msimu wa 1948-1949. Nyota wa Warriors anayeshikilia tuzo ya Mchezaji mwenye Thamani Zaidi-MVP, Stephen Curry alifunga alama 24 katika mchezo huo. Warriors sasa wanawinda kuivunja rekodi ya kushinda mechi 33 mfululizo iliyowekwa na Lakers katika msimu wa kawaida wa NBA mwaka 1972.

No comments:

Post a Comment