Tuesday, November 24, 2015

WENGER KUIPA UZITO EUROPA LEAGUE KAMA LIGI YA MABINGWA.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema ataipa uzito mkubwa michuano ya Europa League kama waking’olewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Arsenal wako wanasuasua katika kundi F wakiwa na alama tatu pekee katika michezo minne waliyocheza na wanatarajiwa kucheza na Dinamo Zagreb baadae leo wakijuwa kuwa wanaweza kutolewa kama wakifungwa. Nafasi ya tatu katika kundi hilo itawapeleka Arsenal katika Europa League na Wenger amesema hadhani kama kushiriki michuano hiyo kutaathiri dhamira yao ya kupigania taji la Ligi Kuu. Akihojiwa Wenger amesema kama kikosi chake kikienguliwa na kwenda kushiriki michuano hiyo ya pili kwa ukubwa barani Ulaya basi hakuna kuwa ataipa uziti unaostahiki.

No comments:

Post a Comment