Tuesday, November 24, 2015

PIGO ARSENAL, COQUELIN NJE MIEZI MIWILI.

KLABU ya Arsenal imepata pigo kufuatia taarifa kuwa kiungo wake Francis Coquelin anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi miezi miwili kutokana na majeruhi ya goti. Meneja wa Arsenal Arsene Wenger alitangaza kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 alipata majeruhi hayo katika mchezo waliofungwa mabao 2-1 dhidi ya West Bromwich Albion Jumamosi iliyopita. Kiungo huyo sasa anatarajiwa kukosa mechi zote za mwezi ujao lakini Wenger ana matumaini makubwa kuwa ataweza kurejea uwanjani mapema kuliko inavyodhaniwa kutokana na vipimo alivyofanyiwa. Katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Wenger atakuwa na nafasi ya kusajili kiungo mwingine kuziba nafasi hiyo lakini mwenyewe amesisitiza kuwa tayari ana viungo wa kutosha katika kikosi chake kuziba nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment