Tuesday, November 24, 2015

GERRARD KUICHEZEA TENA LIVERPOOL.

KIUNGO mkongwe wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard anatarajiwa kuichezea tena klabu hiyo lakini katika kikosi cha manguli waliowahi kuichezea timu hiyo. Nahodha huyo wa zamani anatarajiwa kuwepo katika kikosi hicho cha manguli kitakachokwenda jijini Sydney sambamba na wakongwe wenzake kama Jamie Carragher na Ian Rush kwa ajili ya mchezo dhidi ya manguli wa Australia utakaochezwa Januari 7 mwakani. Kwasasa Gerrard yuko likizo kufuatia msimu wa Ligi Kuu ya marekani-MLS kumalizika ambapo anatarajiwa kurejea tena nchini humo Januari 15 wakati timu yake ya Los Angeles Galaxy itakapoanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya. Akihojiwa Gerrard amesema ni jambo kubwa kucheza katika kikosi rasmi cha wachezaji wakongwe hivyo ana hamu kubwa kukutana na wenzake ambao aliwahi kucheza nao. Mkongwe huyo aliendelea kudai kuwa mashabiki wa Liverpool ni bora na kucheza mbele yao tena litakuwa jambo la kipekee.

No comments:

Post a Comment