Tuesday, November 24, 2015

RONALDO HAENDI KOKOTE - MENDES.

WAKALA wa mshambuliaji Cristiano Ronaldo, Jorge Mendes amesema litakuwa suala lisilowezekana kwa nyota huyo wa kimataifa wa Ureno kuondoka Real Madrid na kuhamia Paris Saint-Germain –PSG wakati Monaco wakiamini kuwa hawana nafasi ya kumsajili. Ronaldo mwenye umri wa miaka 30, alizomewa na mashabiki wakati walipopokea kichapo cha mabao 4-0 kutoka Barcelona katika Uwanja wa Santiago Bernabeu, hivyo kuongeza tetesi za mustakabali wa nyota huyo. Miezi ya hivi karibuni, Ronaldo anayeongoza kwa mabao katika labu hiyo amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia kwa mabingwa hao wa Ufaransa lakini Mendes amekuwa akisisitiza kuwa Ronaldo atabakia nchini Hispania mpaka atakapotundika daruga zake. Akihojiwa kuhusiana na tetesi hizo Mendes amesema ni suala lisilowezekana kwa Ronaldo kuondoka Madrid kwania anatarajia kumalizia soka akiwa hapo.

No comments:

Post a Comment