Tuesday, November 24, 2015

PSG KUVAA JEZI MAALUMU KUKUMBUKA WALIOPOTEZA MAISHA KATIKA MASHAMBULIO YA PARIS.

WACHEZAJI wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG wanatarajiwa kuvaa fulana maalumu katika mechi zao mbili zitakazokuja kwa ajili ya kutoa heshima zao kwa wale waliofariki katika mashambulio ya kigaidi jijini Paris. Fulana hizo zitakuwa na ujumbe maalumu wenye maandishi ya kifaransa yanayosomeka kama Je suis Paris wakimaanisha mimi ni Paris. Mabingwa hao wa Ufaransa wamedai kufanya hivyo ili kuonyesha umoja wao pamoja na jamii ya kimataifa ya soka. PSG watakwaana na Malmo ya sweden katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kesho kabla ya kuikaribisha Troyes katika mchezo wa Ligue 1 Jumamosi hii.

No comments:

Post a Comment