Friday, November 20, 2015

WIMBO WA TAIFA WA UFARANSA KUPIGWA KATIKA MECHI ZA LIGI KUU.

WIMBO wa taifa wa Ufaransa wa La Marseillaise, unatarajiwa kupigwa kabla ya mechi zote za Ligi Kuu ya Uingereza mwishoni mwa wiki hii. Wimbo huo utaimbwa baada ya sarafu kurushwa kuamua nani ataanzisha mchezo, huku wachezaji wa timu zote mbili wakikusanyika kwenye duara katikati ya uwanja pamoja na waamuzi. Afisa mkuu wa Ligi ya Kuu Richard Scudamore amesema hatua hiyo ni ya kuunga mkono Ufaransa na kutoa heshima kwa wahanga wa tukio ya mashambulio ya kigaidi yaliyotokea huko Paris na kuuwa watu zaidi ya 129 Ijumaa iliyopita. Wimbo wa La Marseillaise pia ulichezwa wakati wa mechi ya kirafiki ya kimataifa kati Uingereza na Ufaransa Jumanne katika Uwanja wa Wembley ambapo wenyeji Uingereza walishinda mabao 2-0. Kuna wachezaji 72 wanaocheza katika Ligi Kuu ambao wanatoka Ufaransa.

No comments:

Post a Comment