Friday, November 20, 2015

NITASHINDA VITA YA SARATANI - CRUYFF.

NGULI wa zamani wa soka wa Uholanzi, Johan Cruyff amesema ana imani kubwa atashinda mapambano yake dhidi ya maradhi ya saratani ya mapafu yanayomsumbua. Nguli huyo mwenye umri wa miaka 68 na mshindi wa tuzo tatu za Ballon d’Or aligundulika maradhi hayo mwezi uliopita. Akihojiwa Cruyff ambaye amewahi kucheza na kuwa kocha katika klabu za Ajax Amsterdam na Barcelona, amesema ana uhakika kila kitu kitakwenda sawa kwani anajisikia vyema. Cruyff aliendelea kudai kuwa matibabu ya mionzi aliyoanza ameyafanya kuwa rafiki yake kwasababu yanakwenda kuua maradhi hayo. Nguli huyo aliisaidia nchi yake Uholanzi kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1974 ambapo walifungwa na Ujerumani Magharibi.

No comments:

Post a Comment