Friday, November 20, 2015

SINA MPANGO WA KUREJEA LIVERPOOL AU KLABU YEYOTE ULAYA - GERRARD.

NAHODHA wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard amesema kuwa hatarajii kusaini mkataba Anfield au klabu yeyote nyingine barani Ulaya Januari mwakani. Gerrard mwenye umri wa miaka 35, alijiunga na Los Angeles Galaxy baada ya mkataba wake kumalizika Liverpool majira ya kiangazi na msimu wake wa kwanza Ligi Kuu ya Marekani-MLS umemalizka hivi karibuni baada ya timu yake kumaliza katika nafasi ya tano katika Ukanda wa Magharibi. Nahodha huyo wa zamani wa Uingereza amekuwa akihusishwa na tetesi za kufanya usajili wa muda Liverpool wakati huu ambao msimu MLS umemalizika lakini Gerrard alirudia kauli kama aliyotoa meneja wa klabu hiyo Jurgen Klopp kuwa hatarejea kuitumikia timu hiyo. Gerrard amesema ameshastaafu kuitumikia timu ya taifa hivyo hana chochote cha kuonyesha barani Ulaya. Mkongwe huyo aliendelea kudai kuwa anachotaka hivi sasa ni kupumzika kwasababu anakabiliwa na msimu mrefu mwakani hivyo ni muhimu kwake kurejea akiwa imara.A

No comments:

Post a Comment