BEKI wa Manchester City, Pablo Zabaleta ana matumaini ya kurejea uwanjani wakati watakapokwenda kukwaana na Liverpool Novemba 21 mwaka huu. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina, amekosa mechi saba za City zilizopita baada ya kutolewa nje katika mchezo dhidi ya Newcastle United mwezi uliopita kutokana na majeruhi ya goti. Lakini Zabaleta sasa ana matumaini ya kurejea katika kikosi cha kwanza cha City katika mchezo dhidi ya Liverpool. Akihojhiwa Zabaleta amesema amekuwa akiendelea vyema na amekuwa akijitahidi kujiweka fiti kabla ya mchezo na Liverpool ambao utafanyika baada ya mapumziko kupisha mechi za kimataifa.
No comments:
Post a Comment