KLABU ya Lille ya Ufaransa, imemtimua kazi meneja wake Herve Renard ikiwa haijafika hata miezi sita toka ateuliwa kuchukua kibarua hicho. Hatua hiyo ya Lille imekuja kufuatia timu hiyo kusuasua toka kuanza kwa msimu huu wakiwa wako nafasi moja juu ya eneo la kushuka daraja. Renard mwenye umri wa miaka 47 raia wa Ufaransa, ambaye aliiongoza Ivory Coast kunyakuwa taji la Mataifa ya Afrika Februari mwaka huu, aliteuliwa Mei kuchukua nafasi ya kocha aliyeondoka Rene Girard. Lille kwasasa inashikilia nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligue 1 baada ya kucheza mechi 13 huku mchezo wa mwisho wa Renard ukiwa ni sare ya bao 1-1 waliopata dhidi ya Bastia mwishoni mwa wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment