Sunday, December 20, 2015

BARCELONA YAICHAPA RIVER PLATE NA KUNYAKUWA KOMBE LA KLABU YA DUNIA.

KLABU ya Barcelona imeshinda taji lake la tano kwa mwaka huu baada ya kunyakuwa Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia kwa mara ya tatu kufuatia ushindi mnono waliopata dhidi ya River Plate katika mchezo wa fainali. Katika mchezo huo uliofanyika jijini Yokohama mapema leo, River Plate ya Argentina ilionekana kushindwa kabisa kuendana na kasi ya washambuliaji watatu wa Barcelona Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar na kujikuta wakichapwa mabao 3-0. Messi alifunga bao la kuongoza katika mchezo huo baada ya kurejea tena kufuatia kusumbuliwa matatizo ya figo ambayo yalimfanya kuukosa mchezo wa nusu fainali. Mabao mengine ya Barcelona yalifungwa na Suarez ambaye amemaliza mashindano hayo akiwa na mabao matano baada ya kufunga hat-trick katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Guangzhou Evergrande ya China.

No comments:

Post a Comment