Sunday, December 20, 2015

ANCELOTTI ASHUKURU KUPEWA NAFASI BAYERN.

MENEJA Carlo Ancelotti amejibu kufuatia kuthibitishwa meneja mpya ajaye wa Bayern Munich msimu ujao akieleza kuwa uteuzi huo ni heshima kubwa kwake. Bayern walithibitisha kuwa meneja Muitaliano ambaye amekuwa bila kibarua toka Mei mwaka huu alipotimuliwa na Real Madrid, atachukua nafasi ya Pep Guardiola anayeondoka mwishoni mwa msimu. Akihojiwa Ancelotti amesema ni heshima kubwa kwake kuwa sehemu ya klabu hiyo kubwa msimu ujao kwani wakati alipotambua kuwa wanamtaka alizuia kusikiliza ofa zingine zote. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa anaitakia Bayern pamoja na rafiki yake Guardiola msimu mzuri.

No comments:

Post a Comment