Sunday, December 20, 2015

ANCELOTTI KUCHUKUA NAFASI YA GUARDIOLA BAYERN.

MENEJA wa Bayern Munich, Pep Guardiola anatarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu na nafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa na Carlo Ancelotti. Guardiola mwenye umri wa miaka 44, anahusishwa na tetesi za kwenda katika klabu Ligi Kuu zikiwemo Manchester City, Manchester United, Chelsea na Arsenal. Meneja huyo w zamani wa Barcelona ameshinda mataji mawili ya Bundesliga na moja la Kombe DFB toka ajiunge na Bayern kiangazi mwaka 2013. Ancelotti mwenye umri wa miaka 56, ambaye amekuwa mapumzikoni toka atimuliwe na Real Madrid Mei mwaka huu, amesaini mkataba wa miaka mitatu na Bayern. Mabingwa hao wa Ujerumani kwasasa wanaongoza Bundesliga kwa tofauti ya alama nane na wanatarajiwa kucheza Juventus ya Italia katika hatua ya timu 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ofisa mkuu wa bayern Karl-Heinz Rummenigge amemshukuru Guardiola kwa kila alichoipa klabu hiyo toka alipotua mwaka 2013 na ana matumaini kuwa atawaongezea mataji zaidi katika muda huu aliobakiza kabla hajaondoka.

No comments:

Post a Comment