Wednesday, December 2, 2015

BENITEZ NAYE AMPUMZISHA RONALDO.

MENEJA wa Real Madrid, Rafa Benitez anatarajia kumpumzisha nyota wake Cristiano Ronaldo katika mchezo wa Kombe la Mfalme baadae leo ambapo watacheza dhidi ya timu ya daraja la tatu ya Cadiz. Ni mara chache sana kumuona mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno kuona akikaa nje na mara nyingi amekuwa akiepuka majeruhi pamoja na kipindi kirefu anachocheza. Benitez amesema amefanya hivyo ili kutoa mwanya kwa kikosi kufanya mzunguko na wachezaji wengine wapate nafasi ya kutoa mchango wao katika timu. Wachezaji watano kutoka katika kikosi B cha timu hiyo maarufu kama Castilla wameitwa katika mchezo huo utakaochezwa katika Uwanja wa Ramon de Carranza lakini jina la Ronaldo halipo katika orodha ya wachezaji 17 walioitwa.

No comments:

Post a Comment