RAIS wa Shirikisho la Soka la Liberia, Musa Bility amekata rufani Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS bada ya kuenguliwa katika kinyang’anyiro cha urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Bility alienguliwa katika kinyang’anyiro hicho na kamati ya ya uchaguzi ya FIFA baada ya kushindwa kutimiza baadhi ya vigezo vilivyowekwa. Katika taarifa yake Bility amesema uamuzi huo wa FIFA sio wa haki ndio maana ameamua kukata rufani ili aweze kupata haki yake anayostahili. Moja ya vigezo vinavyodaiwa kumuangusha Bility ni uchunguzi ili kubaini ukweli kuhusu uadilifu wake jambo ambalo amesema alikubali kwa masharti kwamba suala hilo lifanyike katika njia sahihi ili waweze kutoa haki kwa uwazi. Bility pia alitaka FIFA kutoa matokeo waliyopata kwa kila mgombea wa nafasi hiyo kwa wanachama wake kuliko kuficha kama walivyofanya sasa.
No comments:
Post a Comment