WAZIRI mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls amedai kuwa mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema hana nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo. Benzema anachunguzwa kwa tuhuma za kuhusika kutaka hela kwa nguvu kutoka kwa mchezaji mwenzake Mathieu Valbuena lakini alikanusha kufanya jambo lolote baya. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye amefunga mabao 27 akiwa na Ufaransa, anakabiliwa na mashitaka ya kula njama na usaliti kuhusiana na kashfa ya mkanda wa ngono. Valls amesema mwanamichezo mkubwa anapaswa kuwa mfano mzuri na Benzema hayuko hivyo hivyo hawezi kuwa nafasi katika timu ya taifa. Sakata hilo la mkanda wa ngono ambao unadaiwa kumuhusisha Valbuena na mpenzi wake pia lilipelekea nyota mwingine wa nchi hiyo Djibril Cisse naye kuhojiwa na polisi.
No comments:
Post a Comment