KLABU ya Queens Park Rangers-QPR imeanza mazungumzo na kocha wa Burton Jimmy Floyd Hasselbaink ili aje kuinoa timu hiyo. QPR wanaoshiriki ligi daraja la kwanza walituma maombi rasmi kwa Burton kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kocha huyo mwenye umri wa miaka 43 ambaye amewahi kucheza katika klabu za Leeds United na Chelsea. Neil Warnock amekuwa kocha wa muda wa QPR toka Chris Ramsey alipotupiwa virago vyake Novemba 4 mwaka huu. Hasselbaink raia wa Uholanzi amefanikiwa kushinda taji la ligi daraja la pili akiwa na Burton msimu uliopita, na sasa wanaongoza katika msimamo wa ligi daraja la kwanza kwa tofauti ya alama mbili.
No comments:
Post a Comment