MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi anatarajiwa kuukosa mchezo wa Kombe la Mfalme baadae leo ambapo watachuana dhidi ya Villanovense katika Uwanja wa Camp Nou lakini meneja Luis Enrique amewajumuisha Luis Suarez na Neymar katika kikosi chake. Baada ya kupona majeruhi Messi alirejea uwanjani katika kipindi cha pili akitokea benchi katika mchezo wa Clasico dhidi ya Real Madrid Novemba na baadae kuanza toka mwanzo katika michezo dhidi ya AS Roma na Real Sociedad. Hata hivyo, Enrique ameamua kutohatarisha kumtumia nyota huyo wa kimataifa wa Argentina katika mchezo huo dhidi ya timu hiyo ya daraja la tatu, kufuatia kukaa nje kwa miezi miwili akiuguza majeraha ya goti. Suarez na Neymar wanaweza kuchezeshwa baada ya kujumuishwa katika kikosi cha wachezaji 16 katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment