Wednesday, December 2, 2015

MWAMUZI ALIYETIWA "VITASA" NA MASHABIKI AFUNGIWA.

MWAMUZI wa Thailand ambaye alishambuliwa na mashabiki wenye hasira wa klabu ya ligi daraja la tatu kufuatia kufungwa, amefungiwa miezi sita kutokana na uchezeshaji mbaya katika mchezo huo. Mwamuzi huyo Pichit Thongchanmoon alivamiwa na mashabiki wa timu ya Satun United kufuatia kufungwa bao bao 1-0 nyumbani na Khoh Kaen United Novemba 22 mwaka huu. Satun walifungiwa miaka mitatu wiki iliyopita kwa tukio hilo lakini kamati ya Chama cha Soka cha Thailand imesema Pichit alifanya makosa kadhaa katika mchezo huo na kumlima adhabu hiyo. Kamati hiyo imesema Pichit alitakiwa kuipa Satun penati na kuwa mwamuzi huyo alikuwa mbali na eneo husika mara nyingi.

No comments:

Post a Comment