MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Karim Benzema amezungumza na wana habari kwa mara ya kwanza toka atuhumiwe kusaidia kumsaliti mchezaji mwenzake katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa Mathieu Valbuena kwa mkanda wa ngono. Nyota huyo amesema hana hatia yeyote akisisitiza kuwa madhumuni yake makubwa wakati wa kashfa hiyo ilikuwa ni kumsaidia Valbuena kumaliza tatizo lake hilo. Benzema aliendelea kudai kuwa alisikia kuhusu mkanda huo wa ngono unaomhusisha Valbuena na kukwambia anaweza kumsaidia kwasababu ana rafiki huko Lyon ambaye anaweza kukabiliana na matatizo kama hayo. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa hakuzungumza chochote na Valbuena kuhusu fedha kwani analipwa vizuri hivyo akitaka kumsaidia mtu hahitaji chochote kutoka kwake. Benzema amesema hawafahamu kabisa watu waliokuwa wakimsumbua Valbuena wakimtaka kutoa fedha ili wasizambaze mkanda huo.
No comments:
Post a Comment